Dar es Salaam, Tanzania – 17 Juni 2025
Vivo Energy Tanzania, wasambazaji rasmi wa mafuta na vilainishi vya chapa ya Shell, imezindua rasmi kampeni yake mpya ijulikanayo kama “Uliza Oili ya Shell” – harakati kabambe inayolenga kuwaelimisha madereva wa Tanzania kuhusu umuhimu wa kutumia vilainishi halisi vya ubora wa juu kwa ajili ya ufanisi wa injini na maendeleo ya kijamii.
Uzinduzi huo ulifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Masaki, Dar es Salaam, na ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo madereva, waendesha bodaboda, mafundi na wasafirishaji kutoka sekta tofauti. Kampeni hii inalenga kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu vilainishi wanavyotumia ili kulinda injini, kupunguza gharama za matengenezo, na kuongeza ufanisi wa matumizi ya mafuta.
Bw. Mohamed Bougriba, Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, alisisitiza dhamira ya kampeni hiyo wakati wa uzinduzi:
“Tunafurahi kuanzisha kampeni ya ‘Uliza Oili ya Shell,’ kama sehemu ya dhamira yetu kuwahudumia Watanzania kwa vilainishi bora zaidi duniani. Tunaamini kutumia vilainishi sahihi ni hatua muhimu ya kulinda injini, kuongeza ufanisi wa mafuta, na kupunguza gharama kwa muda mrefu.”
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wa Shell duniani:
“Tunawashukuru wateja wetu wote waliotufanya kuwa chapa namba moja ya vilainishi duniani kwa miaka 18 mfululizo. Mafanikio haya ni matokeo ya ushirikiano wa karibu na watengenezaji wakubwa wa magari duniani pamoja na wateja wetu waaminifu.”
Katika hatua ya kusisimua, Bw. Bougriba alitangaza ushirikiano mpya na VETA:
“Kwa kushirikiana na VETA, tunawajengea vijana uwezo wa kitaalamu kwenye huduma za vilainishi – jambo linalochangia ajira, ujasiriamali, na maendeleo ya kweli. Tunawapongeza wahitimu waliopo nasi leo kama ushahidi wa mafanikio ya haraka baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU).”
“Kama methali ya Kiswahili inavyosema, ‘Samaki mkunje angali mbichi,’ tunawekeza mapema kwa vijana wetu kwa ajili ya taifa lenye mafanikio ya kudumu. Na tukikumbuka kauli ya Baba wa Taifa, ‘Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu,’ tunathibitisha kuwa kwa kushirikiana, tunaweza kujenga jamii imara na yenye mafanikio
Bidhaa Kuu Zinazohusika
Kampeni ya Uliza Oili ya Shell inaleta umakini mpya kwa vilainishi vitatu vya Shell:
Shell Advance – Kwa pikipiki, bodaboda, na bajaji; hutoa ulinzi wa hali ya juu kwa injini katika mazingira yoyote.
Shell Helix – Kwa magari ya petroli; huongeza nguvu ya injini, hupunguza uchakavu na hutoa ufanisi wa hali ya juu.
Shell Rimula – Kwa magari ya dizeli kama malori na daladala; hutoa ulinzi wa kudumu na utendaji thabiti kila safari.
Bw. Godwin Mwita, Mkuu wa Biashara ya Vilainishi Vivo Energy Tanzania, alisema:
“Vilainishi vyetu vinapambana na bidhaa bandia kwa kuhakikisha ubora wa hali ya juu. Tumeongeza maeneo ya upatikanaji kote nchini – mijini na vijijini – ili kila dereva aweze kupata Shell ya kweli.”
Kampeni hii itatekelezwa kupitia warsha kwa mafundi, ziara za gereji, mafunzo ya moja kwa moja, na shughuli za kijamii katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na mingineyo
Dkt. Aileen Meena, Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Miradi ya Jamii, alisisitiza:
“Kampeni hii si ya kibiashara pekee bali ni jitihada ya kijamii. Tunajenga uelewa, tunakuza ujuzi wa vijana, na tunaimarisha maisha ya jamii. Hii ndiyo Vivo Energy – kampuni inayojali, kushirikiana, na kuleta maendeleo ya kweli.”
Kwa upande wake, Mdillah Osward, Mratibu wa Kozi Fupi na Uzalishaji wa VETA, alisema:
“Vivo Energy imeonesha dhamira ya kweli – si maneno tu, bali vitendo vinavyoleta matokeo. Ushirikiano huu unatuwezesha kutoa mafunzo yenye tija kwa soko la ajira la sasa.”
Kwa kampeni ya Uliza Oili ya Shell, Vivo Energy Tanzania inaonesha kuwa nishati bora ni ile inayolinda injini, kuinua maisha ya watu, na kuchochea maendeleo ya taifa.
Hakuna maoni: