Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Dkt. Bill Kiwia amewasisitiza waombaji mikopo wote kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 kusoma na kuzingatia miongozo ya utoaji mikopo ili kuwasilisha maombi yao kwa usahihi.
Dkt. Kiwia ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo (Alhamisi, Juni 19, 2025) katika ofisi za HESLB kanda ya mashariki zilizopo jijini Dar es salaam, ambapo ameweka wazi kuwa miongozo hiyo inapatikana kwenye tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz). Dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2025/2026 lipo wazi toka Juni 15, 2025 hadi Agosti 31 mwaka huu.
HESLB imejipanga kutoa huduma kwa waombaji mikopo kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa namba 0736 66 55 33 na kupitia ujumbe wa WhatsApp tu kwa namba 0739 66 55 33 kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni. Katika mwaka wa masomo 2025/2026, Serikali imetenga kiasi cha TZS 917 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya kati na vya elimu ya juu nchini, ambapo itawanufaisha wanafunzi 252,773, kati yao takribani wanafunzi 88,000 watakuwa wa mwaka wa
Hakuna maoni: