JESSICA: CCM INAJALI UONGOZI WA VIJANA


Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA Ndg. Jessica Mshama amesema Chama Cha Mapinduzi kinajali sana uwezo wa Vijana katika uongozi ndio maana kinawaamini na kuwapa nafasi za juu za kiuongozi.


Ndg. Jessica ameonesha uthabiti wa CCM katika uongozi wake kwa kuitofaugisha na vyama vingine kutokana na kuwaamini Vijana katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kwamba ushindi wa CCM hautokani kwa bahati mbaya kwa sababu kimejenga zaidi kwa Vijana.


Kuhusu suala la Uchaguzi, Ndg. Jessica Mshama amesema kuwa Viongozi wa Juu wa Jumuiya ya UVCCM wamekuwa wakiratibu Mikutano inayohusisha Ziara zao katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandaa kupiga kura ifikapo Oktoba 2025.


Ndg. Jessica Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika Jana 08 Julai, 2025 katika studio za Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.


"Vijana Tunasema OKTOBA TUNATIKI ✅"


#KaziNaUtuTunasongaMbele

#TunazimaZoteTunawashaKijani

#OktobaTunatiki✅✅✅

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.