NA: MWANDISHI WETU
DAR ES SALAAM
Mke wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli, ametembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA), yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Mama Janeth alipokelewa na viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na kutembelea banda hilo ili kujionea namna ambavyo ofisi hiyo inavyotoa huduma kwa wananchi kupitia idara, vitengo na taasisi mbalimbali zilizo chini yake.
Miongoni mwa huduma zinazotolewa na ofisi hiyo ni pamoja na:
Miongoni mwa huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu ni pamoja na:
• Elimu kuhusu usimamizi wa maafa
• Shughuli za Wakala wa Kupigachapa Mkuu wa Serikali
• Huduma za Baraza la Taifa la Biashara
• Elimu ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji
• Masuala yanayohusu vyama vya siasa nchini
• Elimu kuhusu VVU na UKIMWI
• Usalama na afya mahali pa kazi
• Huduma kwa watu wenye ulemavu
• Programu ya ASDP II (Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili)
• Fursa kwa vijana
• Huduma kutoka taasisi kama NSSF, PSSSF, WCF na CMA
Mama Janeth alionyesha kufurahishwa na jitihada za serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu katika kutoa huduma kwa wananchi na kuhimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kufaidika na elimu na huduma zitolewazo katika maonesho hayo.
Hakuna maoni: