UHIGWE - KIGOMA
Wilaya ya Buhigwe, nyumbani kwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango walijumuika kwa wingi kumpokea mgombea kiti cha Rais kupitia chama cha Mpainduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana katika wilaya ya Buhigwe ikiwa ni mkutano wa tatu kwa siku hiyo wa Mhe. Dkt. Samia katika Mkoa wa Kigoma. Mhe Dkt. Samia alitumia mkutano huo kuwaeleza wananchi wa Buhigwe na mkoa wa Kigoma yaliyofanyika katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake na kisha yale anayotarajia kuyatekeleza katika kipindi kijacho cha 2025-2030 na kuwaomba wananchi kumchagua yeye na wagombea wengine wa CCM.
TUTAWAINUA WAKULIMA ASEMA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Mgombea wa kiti cha Rais kupitia CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaahidi wanachi wa Buhigwe mkoani Kigoma kuendelea kukiamini na kukichagua chama cha Mapinduzi na wagombea wake wote katika nafasi ya Urais, ubunge na udiwani ili kuendeleza miradi na masuala yote muhimu ya sekta ya kilimo katika wilaya ya Buhigwe. Mbali na kuelezea miradi muhimu iliotekelezwa chini ya usimamizi wa CCM, Mgombea Urais ameahidi kujenga maghala ya kuhifadhia mazao katika wilaya ya Buhigwe. Pia endapo akipewa ridhaa ya kuliongoza taifa katika kipindi kingine cha miaka mitano ataendeleza sera yake ya kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima. Sambamba na hili Dkt. Samia amesema serikali yake imepanga kufungua mashamba mapya mahsusi yanayotegemea kilimo cha umwagiliaji chini ya program ya Jenga kesho yako bora (BBT) mahsusi kwa ajili ya vijana kujiajiri sambamba na ujenzi wa viwanda vidogo ili kuongeza thamani kwa mazao ya tangawizi.
VITONGOJI VYOTE VYA BUHIGWE KUWA NA UHAKIKA WA MAJI - DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Mgombea wa Urais kupitia CCM Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Buhigwe kuwakamilishia usambazaji wa maji katika vitongoji vyote ambavyo havijifikiwa na huduma za maji. Mhe. Samia amesema katika kipindi kilichopita cha miaka minne ya uongozi wake serikali yake imefikisha huduma za maji Buhigwe na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 84 na kuwaomba wananchi kumchagua sambamba na wawakilishi wengine wa CCM ili kukamilisha miradi ya maji inayoendelea katika jimbo la Buhigwe.
MEGAWATI 46 KUZALISHWA MALAGARASI KUONGEZA NISHATI YA UHAKIKA BUHIGWE - DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Wananchi wa Buhigwe mkoani Kigoma wameombwa kumchagua mgombea wa kita cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi mkuu ujao wa oktoba mwaka huu ili aweze kukamilisha miradi ya nishati ya umeme. Akiwa jukwaani Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaomba wananchi wa jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma kumchagua ili kuhakisha Buhigwe inaendelea kuimarika. Alitumia mkutano huo kuwakumbusha namna alivyofanya mapinduzi ya katika sekta ya nishati mkoani Kigoma kwa kuwa ndiye kiongozi wa kwanza katika historia ya Tanzania kuunganisha mkoa wa Kigoma kwenye gridi ya taifa ya umeme mwaka 2022 iliyokuwa inagharimu Taifa jumla ya shilingi bilioni zaidi ya 57 kwa mwaka. Kuhusu ya wilaya ya Buhigwe amesema mengi ameyafanya ikiwemo kuinganisha Buhigwe na mradi wa umeme wa nyakanazi.
Sambamba na hili kupitia REA amesema serikali imetekeleza miradi 43 ya zaidi ya shilingi bilioni 3 iliyotumika kusambaza umeme katika vijiji vyote vya wilaya ya Buhigwe na vitongoji vingi ambapo kwa sasa ni vitongoji 12 tu havijafikiwa na huduma ya umeme. Katika kipindi kijacho serikali yake itazalisha megawati 46 katika mto Malagarasi ambao utasaidia viwanda vidogo kuzalisha kwa uhakika.
AFYA YA WANACHI NI KIPAUMBELE CHANGU CHA KWANZA ASEMA DKT. SAMIA
Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kipaumbele chake cha kwanza kwa wanachi ambapo amesema afya ya wananchi anaowaongoza ni kipaumbele chake cha kwanza. Mhe Samia ameyasema hayo akiwa katika mkutano wa kampeni za kusaka kura za Urais na ya wawakilishi wengine kupitia CCM katika jimbo la Buhigwe. Dkt. Samia ameleza kuwa mpango wake na chama kitaifa ndani ya siku 100 ni kuajiri watalaam wa afya 5000 ambapo amesema Buhigwe watanufaika na watalaam hao. Sambamba na hili Mhe. Dkt. Samia asema katika kipindi kijacho serikali itaanza kutekeleza sheria ya Bima ya afya kwa wote ambapo itaanza mpango wa utekelezaji wake katika siku 100 za mwanzo za muhula wa pili kwa majaribio. Kwa wale wananchi wenye kipato cha chini serikali itabeba gharama zao.
BUHIGWE KUWA NA MAWASILIANO YA UHAKIKA - DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Chama cha Mapinduzi kimewaomba wananchi wa wilaya ya Buhigwe katika mkoa wa Kigoma kuendelea kukipa ridhaa chama hicho ili kiwaletee huduma za mawasiliano ya simu sambamba na huduma ya upatikanaji wa redio ya shirika la utangazaji Tanzania TBC. Hayo yamesemwa na mgombea wa kiti cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa wilayani Buhigwe katika kampeni za uchaguzi leo September 13 mwaka 2025.
TUTAMARISHA MIUNDOMBINU BUHIGWE - MHE. SAMIA SULUHU HASSAN
Mgombea wa kiti cha Rais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameomba wananchi wa jimbo la Buhigwe kumchagua yeye na wagombea wengine wanaotokana na CCM katika uchaguzi mkuu ujao ili kuendelea kujenga na kuimarisha miundombinu ya Barabara katika wilaya hiyo. Ambapo amesema Serikali ya CCM itakapopewa ridhaa na wananchi itajenga Barabara za ndani za mji na mitaa ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji akitaja Barabara za Kalela- Buyama-Buhigwe - Katunda. Sambamba na hili Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mbali na ahadi za chama yeye binafsi atafanya jitihada za kusimika mataa katika mji wa Buhigwe ili kuwarahisishia wafanya biashara fursa ya kufanya biashara zao saa 24 za siku. Mhe. Samia pia ameahidi kufanikisha ujenzi wa kituo cha SGR ili kiwapatie fursa wafanya biashara kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na kujipatia faida zaidi katika biashara zao.
Hakuna maoni: