Dar es Salaam, Tanzania – 25 Septemba
Bolt Tanzania kwa fahari imetangaza kuzindua nambari mpya ya punguzo BOLTXSIMBU, kwa heshima ya Alphonce Felix Simbu, aliyefanya historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika Mashindano ya Dunia ya Riadha.
Ushindi wa Simbu umeiweka Tanzania kwenye ramani ya riadha ya kimataifa, sambamba na mataifa yenye nguvu kama Kenya na Ethiopia. Huu si ushindi wa mtu binafsi pekee, bali ni alama ya kitaifa ya ubora na uwezekano.
“Mwaka huu tuliahidi kujaribu tena, na limekuwa jambo kubwa. Nilishangazwa kwa sababu tulishindana na Wakenya, Waethiopia, na hata wao hawakuamini kuwa Mtanzania ameshinda,” alisema Simbu alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam jana, Septemba 23.
Ushindi huo umebeba ujumbe mzito kwa vijana wa Kitanzania kwamba kwa nidhamu na uvumilivu, wanariadha wengi zaidi wa dhahabu wanaweza kuibuka kutoka nchini.
“Vipaji vinastahili kutambulika, na kama Bolt tunaona ushindi wa Simbu ni zaidi ya medali. Ni uthibitisho kwamba vijana wa Tanzania wanaweza kupaa jukwaa la dunia na kung’aa,” alisema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya.
“Kama vile Simbu alivyojizatiti kufanikisha ubora na kufika kwanza kwa kasi na usahihi, Bolt pia imejikita kuwasaidia Watanzania kusafiri kwa ufanisi, kwa gharama nafuu na kwa wakati,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Meneja wa Mahusiano ya Umma wa Bolt Tanzania, Gilbert Ginono, nambari hii maalum ya punguzo imezinduliwa kama njia ya kukuza chapa ya Simbu nyumbani kufuatia ushindi wa kihistoria aliouleta. Kila safari inayowekwa kwa kutumia nambari hii si tu kusherehekea tukio la kitaifa la fahari, bali pia ni uthibitisho wa uwekezaji wa Bolt katika kutambua na kuinua vipaji vya Kitanzania.
Kupitia mpango huu, Bolt inaendeleza dhamira yake ya kusimamia ufanisi, kutoa fursa na kusherehekea ubora — thamani ambazo zimejidhihirisha kupitia mbio za dhahabu za Simbu.

Hakuna maoni: