DKT SAMIA ATEKELEZA ILANI YA CCM KWA KISHINDO, AONGEZA BAJETI KUU YA SERIKALI KUTOKA TRILIONI 34.88 MWAKA 2020/21 HADI TRILIONI 57.04 MWAKA 2025/26


Rais Samia aliongeza trilioni 1.35 Mwaka wa fedha 2021|22.

Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, bajeti kuu ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2021/22 iliongezeka kutoka shilingi trilioni 34.88 (dola bilioni 14.53) mwaka 2020/21 hadi trilioni 36.23 (dola bilioni 15.10), ongezeko la takriban shilingi trilioni 1.35. Hii ni ongezeko la asilimia 3.9 kwa mwaka huo. Ongezeko hili liliimarisha sekta zinazochochea ukuaji wa uchumi (economic drivers). Kwa mfano, bajeti ya kilimo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 229.8 hadi bilioni 294.2, bajeti ya afya ikaongezeka kutoka shilingi bilioni 933 hadi trilioni 1.2, Hatua hii inaonyesha azma ya Rais Samia kuweka rasilimali za kutosha katika kilimo, afya, na elimu ili kuboresha maisha ya wananchi na kukuza maendeleo ya kiuchumi hasa ajira. Hata hivyo, Kitendo cha Rais Samia kuongeza bajeti kwenye sekta zinazochochea uchumi kunalenga kumpa kila Mtanzania maisha bora.


Rais Samia aliongeza trilioni 5.25 Mwaka wa fedha 2022|23.

Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Bajeti Kuu ya Tanzania iliongezeka kutoka shilingi trilioni 36.23 (dola bilioni 15.10) hadi trilioni 41.48 (dola bilioni 17.28), ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.5, sawa na shilingi trilioni 5.25. Ongezeko hili liliongeza pia bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 294.2 hadi bilioni 751.1, bajeti ya afya kutoka trilioni 1.2 hadi trilioni 1.4. Kitendo cha Rais Samia kuongeza bajeti kwenye sekta hizi zinazochochea uchumi kunalenga kumpa kila Mtanzania maisha bora na furaha kwenye nchi yake.


Rais Samia aliongeza trilioni 2.91 Mwaka wa fedha 2023|24.

Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Bajeti Kuu ya Tanzania iliongezeka kutoka shilingi trilioni 41.48 (dola bilioni 17.28) hadi trilioni 44.39 (dola bilioni 18.50), ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.0, sawa na shilingi trilioni 2.91. Ongezeko hili liliongeza pia bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 751.1 hadi bilioni 970.8 bajeti ya afya kutoka trilioni 1.4 hadi trilioni 1.6, Kitendo cha Rais Samia kuongeza bajeti kwenye sekta hizi kunalenga kumpa kila Mtanzania maisha bora na furaha kwenye nchi yake kupitia huduma nzuri na bora.


Rais Samia aliongeza trilioni 5.90 Mwaka wa fedha 2024|25.

Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Bajeti Kuu ya Tanzania iliongezeka kutoka shilingi trilioni 44.39 (dola bilioni 18.50) hadi trilioni 50.29 (dola bilioni 20.95), ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.3, sawa na shilingi trilioni 5.90. Ongezeko hili liliongeza pia bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 970.8 hadi bilioni 1,248.0, bajeti ya afya kutoka trilioni 1.6 hadi trilioni 1.8, Kitendo cha Rais Samia kuongeza bajeti kwenye sekta hizi kunalenga kumpa kila Mtanzania maisha bora na furaha kwenye nchi yake.


Rais Samia aliongeza trilioni 6.75 Mwaka wa fedha 2025|26.

Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Bajeti Kuu ya Tanzania iliongezeka kutoka shilingi trilioni 50.29 (dola bilioni 20.95) hadi trilioni 57.04 (dola bilioni 23.77), ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.4, sawa na shilingi trilioni 6.75. Ongezeko hili liliongeza pia bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 1,248.0 hadi bilioni 1,243., bajeti ya afya kutoka trilioni 1.8 hadi trilioni 2.0, Kitendo cha Rais Samia kuongeza bajeti kwenye sekta hizi kunalenga kumpa kila Mtanzania maisha bora.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.