Ujenzi na Ukarabati wa Meli ya MV Liemba
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, imefanyia ukarabati mkubwa meli ya kihistoria ya MV Liemba inayofanya kazi katika Ziwa Tanganyika. Meli hii ina uwezo wa kubeba abiria 600 na mizigo tani 300, na ukarabati wake umegharimu takriban shilingi bilioni 22.7.
Mradi huu unatarajiwa kuhifadhi urithi wa kihistoria wa usafiri wa majini, kuchochea utalii wa ndani na wa kimataifa, pamoja na kuimarisha uchumi wa mikoa ya magharibi ikiwemo Kigoma.
.jpeg)
Hakuna maoni: