MAFIA BOXING WAANDAA “SPARRING GAME” KUELEKEA KNOCK OUT YA MAMA

 



Dar es Salaam,

Mafia Boxing Promotion imeandaa pambano maalum la (Sparring Game) litakalofanyika Jumapili ya wiki hii kama sehemu ya maandalizi ya mashindano makubwa ya Knock Out ya Mama yanayotarajiwa kuanza mwezi Aprili 25 mwaka huu.

Pambano hilo litakuwa la kimataifa, likiwahusisha mabondia kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kuwapa vijana fursa ya kuonyesha uwezo wao kwenye jukwaa la kimataifa. Mafia Boxing imeeleza kuwa mpango wao ni kuandaa mapambano kila baada ya miezi miwili ili kuwajengea mabondia uzoefu wa kimataifa.

Aidha, michezo hiyo itaingia kwenye rekodi rasmi za mchezo wa ngumi nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mafia Boxing Promotion, Ally Zayumba, amewasihi Watanzania na wadau wa mchezo wa ngumi kuhudhuria kwa wingi pambano hilo litakalofanyika tarehe 15 katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni, ofisi za Mafia Boxing. Kiingilio kitakuwa shilingi 5,000 kwa kila mtu.

Jumla ya mapambano 15 hadi 16 yanatarajiwa kufanyika, huku pambano la kwanza likitarajiwa kuanza saa 10:00 jioni.

Pambano la Sparring Game litakuwa uzinduzi rasmi wa mashindano ya Knock Out ya Mama msimu wa nane.

Kwa upande wao, baadhi ya mabondia akiwemo Frank Shagembe, wamesema wamejiandaa kikamilifu kwa pambano hilo na kwamba ni kipimo muhimu kuelekea Knock Out ya Mama.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.