PPRA YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA KUHUSU MFUMO WA NeST

 


MOROGORO

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) yatoa Mafunzo ya Ushiriki wa Makundi Maalumu katika Mfumo wa NeST kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Ifakara.

Mafunzo hayo yanafanyika leo Februari 20,2026 katika Ukumbi wa Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.

Wakufunzi katika Mafunzo hayo ni Bw. Christopher Masebo na Sogoye Kamanya kutoka PPRA.

Aidha , Mafunzo hayo yanatolewa kwa lengo la kuwasaidia Watumishi hao Kutekeleza vizuri suala Zima la Sheria ya Ununuzi wa Umma na kuwajengea UWEZO Makundi Maalumu kushiriki kwenye Zabuni za Makundi Maalumu kwenye mfumo wa NeST.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.