TWCC YAJIVUNIA MAKUBWA NDANI YA MIAKA 20,MWAJUMA,AGNES NA WAKILI AMNE WAFUNGUKA

 


CHAMA cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kimesema miaka 20 ya chama hicho kimeweza kuwainua wanawake kiuchumi na kuwajengea uwezo wa mitaji.

Hayo yamebainishwa leo mapema jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa TWCC, Mwajuma Hamza,wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya chama hicho.

Amesema wakati wa kuanzishwa chama hicho mwanamke alikuwa anaonekana ni mtu hasiyejiamini ambaye hawezi kufanya kazi yoyote pamoja na mfumo Dume.

"Hizi zilikuwa changamoto baada ya uwezeshaji wetu kupitia jamii ,sahivi tunaona mwamko ni mkubwa,wanawake wanapata safari,wanapata mitaji kwa ajili ya kufungua Biashara zao"Amesema Mwajuma.

Mwajuma amesema TWCC kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na maeneo maalum ya kiuchumi nchini (TISEZA) kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake wa kuzitambua fursa za uwekezaji,

"Hapa tupo na Wataalam wa TISEZA wanawajengea uwezo wanawake waweze kuzitambua fursa za uwekezaji ili waweze kushirikiana katika kujenga Biashara zao"Amesema Mwajuma.

Kwa upande wake ,Agnes Mgongo ambaye ni Mkurugenzi kampuni ya usambazaji wa vitabu nchi,amesema TWCC imeweza kumuinua kiuchumi.

"TWCC nipo nao miaka kumi na tano sasa katika miaka hiyo nimeweza kutembea nchi mbalimbali kujipatia ujuzi wa kukuza biashara ikiwemo kupata ufadhili,na kuchangia kuongeza masoko"Amesema.

Naye Wakili Amne Suedi ambaye ni mshauri wa kisheria na uwekezaji ,ametumia maadhimisho ya miaka 20 ya TWCC kwa kuwapongeza kwa hatua ya kuwainua wanawake kiuchumi.

Wakili Amne ambaye pia ni mwandishi wa vitabu amewaomba wanawake kuacha uoga na kutakiwa kuthubutu kwenye biashara jambo litakalowafanya wainuke kibiashara.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.