Timu ya Mpira wa Kikapu ya Dar City (@darcitybasketball ), ya Tanzania imeendeleza ubabe katika Michuano ya BAL 2026, Nchini Afrika Kusini baada ya kuifunga Nairobi City Thunder kwa vikapu 90-85.
Dar City imeendelea na ubabe kwa kushinda mechi ya pili mfululizo kitu ambacho kimewashangaza hadi Waandaaji kwa sababu ya ugeni wa Tanzania katika michuano hiyo.
Dar City Sasa watarudi tena uwanjani March 31, 2026 na kucheza dhidi ya Al Ahly Benghazi ya Libya.

Hakuna maoni: