Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imetoa cheti cha shukrani kwa Wakala wa Vipimo (WMA) ikitambua mchango wake katika kuwezesha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kimataifa ngazi ya Mkoa.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika Kongwa, Machi 8, 2026, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Rosemary Senyamule amekabidhi cheti hicho chenye sahihi yake.
Mbali na kuchangia fedha kuwezesha maadhimisho hayo, pia WMA iliweka kambi kwenye viwanja vya maadhimisho na kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi.



Hakuna maoni: