PIC YATAKA MRADI WA BRT KULINDWA


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Tatu unaoanzia katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto ziara ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Masanja Kadogosa kwa lengo la kujionea hatua zilizofikiwa katika mradi huo wa kimkakati.

Miradi ya Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka BRTni sehemu ya mipango ya Serikali ya kupunguza msongamano wa magari na kero ya usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam ambayo inatekelezwa katika awami Sita.

Katika ziara hiyo Mhe Kadogosa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati nchini akibainisha kuwa utoaji wa fedha hizo kwa wakati ndio uliowezesha mradi huu wa awamu ya tatu kufikia hatua kubwa ya ukamilishaji ambapo kwa sasa ujenzi wa Vituo na Barabara za zege umeikia asilimia 99%


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.