ACT WAZALENDO YALALAMIKIA BAJETI YA VIJANA, YASEMA BILIONI 28 ZIMEELEKEZWA KWENYE CHAI BADALA YA MAENDELEO

 


DAR ES SALAAM. 

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wake Taifa, Abdul Nondo, kimeonesha kusikitishwa na mgao wa bajeti ya maendeleo ya vijana, kikidai kuwa kipaumbele hakijazingatia mahitaji ya msingi ya vijana nchini.

Nondo amesema kuwa jumla ya shilingi bilioni 28 zimetengwa kwa ajili ya “chai na matumizi mengine ya kiutawala”, huku ni takribani bilioni 4 pekee ndizo zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya vijana, hatua ambayo ameieleza kuwa inakwenda kinyume na matarajio ya vijana wengi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchambua bajeti ya Maendeleo ya Vijana iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, Nondo amesema ACT Wazalendo inaona kuna haja ya serikali kupitia upya mgawanyo huo ili kuhakikisha vijana wananufaika zaidi kiuchumi.

Ameongeza kuwa vijana wengi nchini wanakabiliwa na changamoto ya ajira na mitaji, hivyo bajeti inayowahusu inapaswa kuelekezwa zaidi katika kuwawezesha kiuchumi badala ya matumizi ya kiutawala ambayo hayana mguso wa moja kwa moja kwa maisha yao.

ACT Wazalendo imesisitiza kuwa iwapo fedha hizo zitapangwa upya kwa usahihi, zitasaidia kuongeza fursa za ajira, ujasiriamali na kukuza maendeleo ya sekta ya vijana kwa ujumla nchini.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.