RC CHALAMILA AKABIDHI MWENGE WA UHURU 2026 MKOA WA PWANI

Na Mwandishi Wetu, 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Pwani baada kukimbizwa kwa siku tano katika Mkoa huo ambapo miradi yote ya maendeleo katika wilaya zote 5 za Mkoa wa Dar es Salaam imepitishwa na Mwenge wa Uhuru kwa asilimia 100 hakuna mradi uliokataliwa.

Mwenge wa Uhuru 2026 ulianza kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es salaam April 13, 2026 ukianza Wilaya ya Ilala, April 14, 2026 Kigamboni, April 15, 2026 Temeke, April 16, 2026 Ubungo na April 17,2026 umehitimishwa Wilaya ya Kinondoni ambapo mapema leo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila katika eneo la mkesha viwanja vya Bunju.

Katika Mkoa wa Dar es Salaam Mbio za mwenge wa Uhuru zikiongozwa na Ndg Wazo Michael Mwang'onda Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ameongoza kuukimbiza Mwenge huo umbali wa Km 392.22 ukitembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 35 ya maendeleo yenye thamani zaidi ya Bilioni 113.5 ambapo miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru kwa kishindo hakuna mradi uliokataliwa.

Aidha Mwenge wa Uhuru ukiwa unakimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa umeendelea kuelimisha jamii na kuwahamasisha wananchi kupitia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo "Tanzani ni Yetu Sote Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo" pamoja kuhamasisha wananchi mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Rushwa na mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya.

Mwenge wa Uhuru 2026 leo April 18, 2026 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge ambako utaendelea kutembelea, kukagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.



Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.