TUGHE YASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA KUU TUCTA, KAULI MBIU MEI MOSI YAPITISHWA

Na Yunge Kanuda, 

DODOMA.

Wajumbe wa Baraza kuu la TUCTA wanaotoka katika Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE) wameshiriki kikamilifu katika kikao cha siku mbili cha Baraza Kuu TUCTA kikichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma. 

Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Cde. Joel Kaminyoge ameongoza Wajumbe wengine Kushiriki katika kikao hicho ambapo pamoja na mambo mengine kililenga kupitia na kufanya tathmini ya kazi mbalimbi zilizofanywa na Shirikisho hilo. 

Aidha katika hatua nyingine Kikao hicho kimepitisha Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani - Mei Mosi kwa mwaka 2026 ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Njombe. 

Akitangaza Kauli mbiu hiyo Katibu Mkuu wa TUCTA ambaye pia ndiye Katibu Mkuu wa TUGHE, Cde. Hery Mkunda alieleza kuwa maadhimisho ya mwaka huu ya Mei Mosi yatabeba Kaulimbiu isemayo:

“Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu Katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”

Cde. Mkunda alihitimisha taarifa hiyo kwa kubaisha kuwa Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye tayari ameshathitisha kushiriki.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.