WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGIA MATIBABU YA MOYO

WITO umetolewa kwa WATANZANIA wa Ndani ya Nchi na Nje ya Nchi kuweza kuchangia Miundombinu pamoja na Vifaa Tiba ilikuwezesha Matibabu ya Moyo kuweza kufanyika Hapa Nchini,ilikupunguza Gharama za Rufaa za Matibu hayo Nje ya Nchi.

Wito huo Umetolewa Aprili 09,2026 jijini Dar es Salaam na MKurugenzi wa Hospital ya Kilimanjaro Christian Center (KCMC)Gillian Masenga Wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari Ambapo amesema kuwa hadi sasa wameweza kukusanya Shilingi Bilioni 22 ambapo nisawa na Asilimia 90 ya ujenzi huo amesisitiza Changamoto ni upatikanaji wa Shilingi Bilioni 2.7 Ambapo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo amewataka Watanzania kuitikia wito huo wa Changizo hilo.

" Ujenzi wa jengo Miundombinu na Vifaa ba umegharimu Shilingi takriban Bilioni 22, sawa Asilimia 90 ya ujenzi tunahitaji Shilingi Bilioni 2.7ilikuweza kukamilisha Jengo pamoja Miundombinu "Amesema Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya KCMC Gillian Masenga. 

Masenga Ameongeza kuwa Hospital hiyo inahudumia Matibabu ya Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Magonjwa yamoyo ambayo huchangia Asilimia 70 ya Vifo Duniani. 

Amesisitiza kuwa Magonjwa ya moyo na Mishipa ya Damu ndio chanzo kikuu cha vifo Duniani. 

"Takwimu za Hospital ya KCMC zinaonesha Asilimia 14.4 ya wagonjwa ni wagonjwa wa moyo,ambapo Hulazwa kwa wastani wa siku 9 hadi 10 na Asilimia 38.5 ya wagonjwa wanaoruhusiwa hulazwa tena Hospitalini" Amebainisha Masenga

 Aidha kwa Upande wake Dakitari Bingwa Mbobevu wa idara ya Watoto (KCMC) Dk.Ronald Mbawasi amesemakuwa tafiti zinaonesha kuwa kati watoto 100 watoto watatu wanaofika Hospitalini hapo wanakabiliwa na tatizo la moyo.

Amesema Wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo ya Moyo Huishi wastani miaka 28.

"Takwimu za mwaka 2025 zinaonesha kuwa kati watoto 70,000 walibainika kuwa natatizo la moyo Asilimia 10 ya wagonjwa hao waweza kugundulika mapema" Amesema Mtalamu wa tibaMoyo Hospital ya KCMC Ronald Mbwasi.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.