MNEC NDELE MWASELELA, AUNGANA NA CHAMA WILAYA RUNGWE KUTOA MKONO WA POLE KWA WAHANGA 35 KWA KUWAPATIA MITAJI YA BIASHARA

📍AMSHUKURU MBUNGE MWANTONA KUUNGA MKONO ZOEZI HILO

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndugu Ndele Mwaselela Leo tarehe 27/06/2026 ameungana na Viongozi wa CCM wilaya ya Rungwe kuwatembelea na kuwashika mkono wa pole Wananchi na wafanyabiashara wahanga wa janga la Moto katika Vibanda vya Biashara katika Kata ya Kimo wapatao 35 wakiwemo Mama lishe na Baba lishe.

Aidha Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe Ndugu Meckson Mwakipunga Amempongeza mkuu wa Wilaya kwa kuwa Karibu na wahanga wa janga Hilo la moto na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Mkopo kwa Wahanga wa janga Hilo, na hapa Tayari wamenufaika kwa na Mkopo huo wa asilimia 10 za Halmashauri na kuongezewa mda wa marejesho.

Akizungumza Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndugu Ndele Mwaselela amewapongeza Viongozi wa CCM kwa kuendesha vyema Chama katika Wilaya.

Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mhe. Antony Mwantona kwa kuwa Karibu na Wananchi wake na pia kwa Kuunga Mkono kwa kutoa mchango wake kwa Wahanga hao.

Amezidi kutoa wito kwa wanaCCM kujibu hoja za Wapinzani na kumtetea Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Ndugu Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Ninyi wenyewe mmejionea tumeunguliwa na Moto lakini tunaishi nao hapa Wala hawajajitokeza Kuja kutufariji, ila wanakuja kututukana tuu, si kwamba Sisi CCM tunazo hela nyingi lakini tuu ni Upendo wetu ambao ndio Msingi wa Chama chetu"

Mwisho MNEC Mwaselela, ameweza kutoa pole kwa majanga yote yaliyowapata wanaRungwe na amewasilisha Mitaji Hiyo iliyochangwa na, Kamati ya Siasa ya Wilaya, Ofisi ya Mbunge na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa.


#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.