Imeelezwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka dhamira ya dhati katika kuleta mapinduzi ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia yanayoongozwa na mkakati wa taifa wa Nishati Safi ya kupikia kwa mwaka 2024-2034 unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania wanatumia Nishati Safi ya kupikia ifikapo 2034.
Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba alipokuwa akifunga kongamano la kuhamasisha na kuelimisha juu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia Juni 25, 2026 lilokuwa likifanyika katika Ukumbi wa East Africa Commercial Logistic Center uliopo Jijini Dar es Salam.
Mhe. Salome amesema kuwa ni muda wa kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kuweza kulinda afya pamoja na kutunza Mazingira hali itakayosaidia Nchi kuingia kwenye mapinduzi makubwa ya Matumizi ya Nishati Safi.
"Katika kuhakikisha tunafikia lengo la asilimia 80 mwaka 2034 Serikali imefanya maamuzi mbalimbali ya kisera na kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuondoa au kupunguza kodi mbalimbali kwenye vifaa vya Nishati safi ili kupunguza gharama ya vifaa hivyo kwa mtumiaji wa mwisho" alieleza Mhe. Salome.
"Tutaendelea kuhakikisha tunapata miradi ambayo itatuwezesha kusambaza majiko mengi zaidi kwa wananchi na wateja wetu ili wote tuweze kutumia Nishati Safi ya Kupikia kwa umeme ambayo sisi kama shirika tunazalisha na tunapenda wateja wetu waendelee kutumia"
Aliongeza kuwa tofauti na Nishati Safi ya kupikia kwa Umeme TANESCO imeendelea kuimarika kwa maana ya huduma kwa wateja kwa kuhakikisha wateja wote wanapata taarifa rasmi na sahihi wakati wote.






Hakuna maoni: