MADINI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1.3 YAKAMATWA KAGERA


Kagera

MAMLAKA za serikali nchini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vimefanikiwa kukamata madini ya dhahabu yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.345,998,291.67 yaliyokuwa yakitoroshwa kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Kukamatwa kwa madini hayo kumeeripotiwa kufuatia operesheni ya Julai 1, 2026 iliyofanywa na Tume ya Madini ikishirikiana na Kikosi Kazi cha Kuzuia Utoroshaji wa Madini.

Baada ya utambuzi na uthamanishaji kufanyika ilibainika kuwa idadi ya vipande vya dhahabu vilivyokuwa vikitoroshwa ni 163 vyenye uzito wa gramu 4434.66.

Hayo yamebainishwa leo Julai 13, 2026 mkoani Kagera na Naibu wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Dkt.Kiruswa amesema kuwa, Serikali imejipanga vyema kuendelea kusimamia Sekta ya Madini ili kukabiliana na utoroshaji wa madini unaofanywa na watu ambao sio waaminifu nchini.

Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa, katika kipindi cha mwezi Julai 2025 hadi Machi 2026 , Serikali imefanikiwa kukamata madini yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.31 ambayo yalikamatwa katika matukio 55 nchini kote.

Aidha, taratibu za kutaifisha madini hayo ili yawe mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaendelea.

Dkt.Kiruswa ametoa wito kwa wachimbaji, wafanyabiashara wa madini (dealers na brokers), na wananchi kwa ujumla kutumia masoko rasmi zaidi ya 40 ya madini na vituo vya ununuzi vilivyoanzishwa kote nchini ili kufanya biashara zao kwa usalama, uhuru, na kuchangia maendeleo ya taifa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.