CHALINZE, PWANI.
Utekelezaji wa Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze mkoani Pwani hadi Dodoma umefikia asilimia 94, hatua inayoukaribisha kukamilika kwa moja ya miradi mikubwa ya miundombinu ya umeme inayotarajiwa kuimarisha usafirishaji wa nishati nchini.
Mradi huo wenye urefu wa kilomita 345 na thamani ya takribani shilingi bilioni 514, unaofadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Awamu ya Sita, unatarajiwa kukamilika Agosti 21, 2026.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo, Meneja wa Mradi, Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Irene Gowelle, amesema kazi hizo zitahitaji kuzimwa kwa baadhi ya njia kuu za kusafirisha umeme za kilovolti 220 na 132 ili kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na utekelezaji wa kazi unafanyika kwa ufanisi.
Kwa mujibu wa Gowelle, katizo hilo litahusu baadhi ya maeneo ya Kanda ya Kati, Kaskazini, kanda ya Ziwa, Magharibi na Kusini Magharibi, huku mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara ikiwa haitaathirika.
Amesema kazi hizo zitafanyika kwa awamu mbili, kuanzia Julai 30 hadi Agosti 4 na Agosti 11 hadi Agosti 17, 2026, kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.
Gowelle amesisitiza kuwa hakuna mteja atakayekosa umeme kwa siku zote za utekelezaji wa kazi hizo, kwani ratiba ya katizo itatofautiana kulingana na eneo husika. Ameongeza kuwa wananchi wanashauriwa kufuatilia ratiba zitakazotolewa kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii ya TANESCO na makundi ya WhatsApp ya mikoa.Nafikiri mtindo huu unaipa habari uzito zaidi kwa kuanza na mafanikio na umuhimu wa mradi, kisha baadaye kueleza sababu ya katizo la umeme badala ya kulifanya liwe kiini cha habari tangu mwanzo.
Kwa upande wake Mhandisi Newton Livingston Mwakifwamba, amesema kazi zilizobaki ni za hatua ya mwisho ya kuunganisha njia mpya za kusafirisha umeme kwenye gridi ya taifa.
Ameeleza kuwa maeneo ya Mkambarani, Kikombo na Nkonze yatakuwa kitovu cha kazi hizo, ambapo njia mpya za umeme zitaunganishwa sambamba na miundombinu iliyopo ili kukamilisha mradi huo kwa usalama na ufanisi.
Mhandisi Mwakifwamba amesema kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha TANESCO kusafirisha umeme wote wa megawati 2,115 unaozalishwa katika Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), tofauti na hali ya sasa ambapo uwezo wa kusafirisha ni takribani megawati 850 pekee.
Ameongeza kuwa mradi huo pia utafungua fursa za biashara ya umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kupitia mifumo ya Eastern Africa Power Pool (EAPP) na Southern African Power Pool (SAPP), hivyo kuiwezesha Tanzania kuuza au kununua umeme kutoka nchi jirani kama Kenya, Ethiopia na Zambia.
Kuhusu hudumaza Reli ya Kisasa (SGR), amesisitiza kuwa hakutakuwa na changamoto yoyote na huduma zitaendelea kama kawaida bila kuathiri utendaji wake.




Hakuna maoni: