Mwanza inatarajiwa kuwa kitovu cha wadau wa sekta ya madini nchini wakati Jukwaa la Local Content Compliance Forum (LCCF) 2026 litakapofanyika kuanzia Julai 22 hadi 24, 2026 katika Hoteli ya Malaika Beach Resort.
Jukwaa hilo litafunguliwa rasmi na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony P. Mavunde (Mbunge), likiwa na kaulimbiu isemayo "Jifunze, Unganisha Mitandao na Kuza Biashara Yako katika Sekta ya Madini Tanzania."
LCCF 2026 linatarajiwa kuwakutanisha taasisi za Serikali, kampuni za madini, wazabuni wa ndani, wafanyabiashara wa madini, wawekezaji, watoa huduma kwa migodi pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo katika sekta hiyo.
Washiriki watapata nafasi ya kufuatilia hotuba kuu, mijadala ya jopo, vikao vya kitaalamu na maonesho yatakayowasilisha bidhaa, huduma na teknolojia mbalimbali zinazochochea ukuaji wa sekta ya madini nchini.
Aidha, jukwaa hilo litatoa fursa ya kujenga mitandao ya kibiashara kwa kukutana na viongozi waandamizi wa Serikali, viongozi wa sekta ya madini na wadau muhimu wa kufanya maamuzi, sambamba na kujifunza kuhusu utekelezaji wa maudhui ya ndani (Local Content), mwelekeo mpya wa sekta, sera na mbinu bora za biashara.
Waandaaji wamewahimiza wadau wote kujisajili mapema kupitia tovuti ya lcforum.tumemadini.go.tz ili kushiriki katika jukwaa hilo ambalo linalenga kuimarisha ushiriki wa wazawa na kufungua fursa zaidi za uwekezaji, ushirikiano na ukuaji endelevu wa sekta ya madini nchini Tanzania.
MWANZA SET TO HOST LCCF 2026, UNLOCKING NEW OPPORTUNITIES IN TANZANIA'S MINING SECTOR
Mwanza is set to become the hub of Tanzania's mining industry as the Local Content Compliance Forum (LCCF) 2026 takes place from 22–24 July 2026 at Malaika Beach Resort.
The forum will be officially opened by the Minister for Minerals, Hon. Anthony P. Mavunde (MP) under the theme, "Learn, Connect and Grow Your Business in Tanzania's Mining Sector."
LCCF 2026 will bring together Government institutions, mining companies, local suppliers, mineral dealers, investors, mine service providers and members of the public to explore opportunities for strengthening local participation and promoting sustainable growth in the mining sector.
Participants will benefit from keynote presentations, panel discussions, technical sessions and exhibitions showcasing innovative products, services and solutions that support Tanzania's mining industry.
The forum will also provide a unique networking platform, enabling participants to connect with senior Government officials, mining industry leaders and key decision-makers, while gaining valuable insights into local content implementation, emerging trends, policies and best practices.
Organisers have encouraged all interested stakeholders to register online through lcforum.tumemadini.go.tz and take part in this important event aimed at unlocking new investment, procurement and partnership opportunities across Tanzania's mining sector.

Hakuna maoni: