NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA SABASABA 2026

Na Doris Njau, 

Dar es Salaam.

NAIBU Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mh. Hamad Hassan Chande, leo Julai 6, 2026 ametembelea Banda la Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama SABASABA.

Mh. Chande amepongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi kubwa ya kuhifadhi, kulinda na kuendeleza urithi wa historia, tamaduni na malikale za Taifa, pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa urithi huo katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na utalii.

Aidha, amesisitiza Makumbusho ya Taifa la Tanzania kuendelea kutumia ubunifu na teknolojia katika kutangaza vivutio vya urithi wa utamaduni na historia ili kuwavutia wananchi na watalii wengi zaidi, hususan kuelekea fursa za Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambapo Tanzania itapokea wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Makumbusho ya Taifa la Tanzania inaendelea kuwakaribisha wananchi kutembelea banda lake katika Maonesho ya SABASABA ili kujionea historia ya Tanzania, masalia ya Dainosaria, utamaduni wa Kiswahili, malikale na urithi mwingine wa kipekee unaotambulisha Taifa letu duniani.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.