Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Profesa Palamagamba Kabudi amekagua maandalizi kuelekea Siku ya Mashujaa Julai 25, 2026
ambapo ameleza kuridhishwa na hatua ya kukamilika kwa maandalizi hayo.
Waziri Kabudi, amekagua hii leo 24 Julai, 2026 akiongozana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe Dkt. Rhimo Nyansaho pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Patrobas Katambi katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Aidha, Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.








Hakuna maoni: