TANZANIA NA OACPS WAKUBALIANA KUINUA SEKTA YA UVUVI NA UCHUMI WA BULUU KWA MANUFAA YA WANANCHI WA NCHI WANACHAMA
Tanzania na Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu ili kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi, usalama wa chakula, ajira na ustawi wa wananchi wa nchi wanachama.
Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa kikao kati ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb.), na Katibu Mkuu wa OACPS, Mhe. Moussa Saleh Batraki, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam, tarehe 21 Julai 2026.
Aidha, Waziri Kakurwa amesema kuna umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na kukuza biashara yake ndani na nje ya nchi. Huku akisisitiza haja ya kuharakisha utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa na nchi wanachama ili kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Nyamanga, pamoja na viongozi na watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Sekretarieti ya OACPS.














Hakuna maoni: