MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na haki za Binadamu(LHRC),Dkt Anna Henga,ameyataka mashirika ya haki za Binadamu kujenga mfumo mbadala wa upatikanaji ufadhili kupitia uhisani wa kijamii na uhisani wa ndani, badala ya kutegemea zaidi ufadhili kutoka nje.
Dkt, Henga ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye Kongamano la kimataifa la UHISANI 2026 ambalo lilishirikisha Asasi mbalimbali za Kiraia lenye lengo kujadili mambo mbalimbali.
Akiongoza mjadala wa mazingira wezeshi katika kongamano hilo,Dkt, Henga amesema Kujipanga kwa mabadiliko ya mazingira ya ufadhili. Mashirika ya kiraia yanapaswa kutafuta na kutumia vyanzo mbalimbali vya rasilimali, kuimarisha ushirikiano na kupunguza utegemezi mkubwa wa ufadhili wa kimataifa.
"LHRC imejizatiti kuendeleza mjadala huu kupitia vikao vya mtandaoni, kufuatilia kinachoendelea, wapi, lini na kinafanywa na nani, ili kuwezesha ushirikiano wenye malengo na dhamira zaidi"amesema .
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Foundation For Civil Society,Gabriel Bundala,akichangia kwenye a katika mijadala kuhusu uhisani wa kijamii, uhamasishaji wa rasilimali za ndani na ujumuishaji wa kifedha
Akirejea maarifa na matokeo kutoka katika utafiti wa FCS unaojulikana kama “Beyond the Buzz,” Gabriel amesisitiza umuhimu wa mashirika ya kiraia (CSOs) kuondokana na mahusiano ya ufadhili yanayolenga miamala pekee, na badala yake kujenga ushirikiano wa maana na endelevu na sekta binafsi, unaojengwa juu ya misingi ya kuaminiana, matokeo chanya na thamani ya pamoja.
Katika mkutano huo yalijadiliwa mambo mbalimbali huku mjadala uliongozwa na tafakari kutoka kwa Dkt. Stigmata Ter, Mkurugenzi Mtendaji wa apnafrica, na uliwakutanisha Shaun Samuels (SGS Consulting), Madonna Ainembabazi (Giving Tuesday Africa), Berhanu Demiss (DEC), Eshban Kwesiga (GFCF),
Mambo Muhimu Yaliyojadiliwa ikiwemo
Kuziba pengo kati ya mashirika ya kiraia na sekta binafsi.Mashirika ya kiraia (CSOs) yana uelewa mkubwa kuhusu jamii, lakini ushirikiano imara zaidi unahitaji lugha ya pamoja, ushahidi wa kutosha, pamoja na uelewa mzuri wa namna sekta mbalimbali zinavyoshughulikia maendeleo.
Pia Kutambua utamaduni wa ukarimu uliopo barani Afrika. Kutoa, mshikamano na hatua za pamoja tayari ni sehemu muhimu ya maisha na utamaduni wa jamii zetu. Hivyo, tunapaswa kutambua na kujenga juu ya utamaduni huu uliopo badala ya kuanzisha mifumo mipya kutoka mwanzo.
Pamoja Kubadili mtazamo kuhusu rasilimali za jamii.
Pia Shaun alisisitiza uwezo mkubwa uliopo katika mifumo ya akiba ya jamii. Mifumo kama VICOBA haipaswi kuonekana tu kama vikundi visivyo rasmi, bali itambuliwe kama wahusika muhimu katika kugharamia na kuchochea maendeleo ya jamii.

Hakuna maoni: