CHUO CHA DMI CHAWAITA VIJANA KUJIUNGA,BANDA LAO LAFANA NANENANE



DODOMA

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimewataka vijana wa kike kuchangamkia fursa za masomo katika sekta ya Usafiri maji,kwani chuo hicho kina fursa kwa kupata ajira ndani na nje ya nchi kutokana na mahitaji makubwa ya wataalamu wa sekta hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 4, 2026, Jijini Dodoma na Mkufunzi Msaidizi wa chuo hicho, Baharia Jackline Lema,wakati akizungumza na waandishi wa habari hii, kwenye banda la DMI lilopo kwenye Maonesho ya Kilimo ya NaneNane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma,  

Aidha,Bi Lema amesema ushiriki wa DMI katika maonesho hayo unalenga kutoa elimu kwa umma kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho pamoja na fursa zilizopo katika sekta ya bahari.

Hata hivyo, mtaalamu huyu ameeleza kuwa wanafunzi wanaochagua kusoma ubaharia hawatajutia uamuzi wao kwakuwa taaluma hiyo ina fursa nyingi za ajira ndani ya nchi na nje.

Amefanuna kuwa chuo cha DMI inatoa kozi mbalimbali ikiwemo unahodha, uhandisi ikiwemo mafuta na gesi pamoja na fani nyingine zinazohusiana na sekta ya bahari, amebainisha kuwa mwitikio wa wanafunzi umeendelea kuongezeka kila mwaka, ambapo zaidi ya wanafunzi 2,000 walihitimu katika mwaka wa masomo 2025/2026, jambo linaloonyesha kuongezeka kwa uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa sekta hiyo.

Ameongeza kuwa DMI ni chuo cha serikali kinachopokea wanafunzi wanaokidhi vigezo vya udahili na kwamba dirisha la maombi ya ngazi ya cheti na diploma litafunguliwa rasmi Agosti 23, 2026, huku udahili wa shahada na uzamili ukiendelea kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Vilevile amesema wahitimu wa DMI hupata nafasi za ajira katika taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo TASHICO, TASAC na TPA, kampuni za usafirishaji, kampuni za mafuta na gesi,kampuni za usafirishaji na baadhi ya maeneo mengine ya kazi ndani na nje ya Tanzania kulingana na mahitaji ya soko la ajira duniani.

Akizungumzia dhana iliyokuwepo hapo awali kuwa ubaharia ni taaluma ya wanaume pekee, amesema idadi ya wanawake wanaojiunga na fani hiyo imeongezeka kwa kiwango kikubwa, hali ambayo imeondoa mtazamo huo na kuonyesha kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika sekta ya bahari.

Pia ameeleza namna wanafunzi wa DMI wanavyopata vipaumbele na fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo pamoja na mikopo ya Serikali inayoratibiwa na HESLB, Samia Scholarship kwa baadhi ya programu, mikopo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na METFUND kwa wanaosoma kozi zinazohusiana na ubaharia.

Amesisitiza kuwa wahitimu wa DMI wameendelea kuwa miongoni mwa wataalamu wanaohitajika zaidi katika soko la ajira la kimataifa, jambo linaloifanya sekta ya bahari kuwa chaguo bora kwa vijana wanaotafuta taaluma yenye ajira za uhakika na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.