KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI AIPONGEZA TAA KWA KUIMARISHA HUDUMA ZA VIWANJA VYA NDEGE


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara, ameipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa hatua zinazochukuliwa katika kuboresha na kuimarisha usimamizi wa viwanja vya ndege nchini, ameeleza kuwa maboresho hayo yana mchango mkubwa katika kuchochea shughuli za kiuchumi, ikiwemo sekta ya kilimo.

Profesa Kahyarara ameyasema hayo alipotembelea banda la TAA katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika Jijini Dodoma, ambapo amepata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na TAA pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika viwanja vya ndege nchini.

Akiwa katika banda hilo, Katibu Mkuu ameipongeza TAA kwa utendaji wake katika kusimamia, kuendeleza na kuboresha miundombinu na huduma za viwanja vya ndege, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuweka nguvu katika sekta ya usafiri wa anga ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa Watanzania.

"Serikali inaendelea kuwekeza na kuweka nguvu kubwa katika kuboresha viwanja vya ndege katika maeneo mbalimbali nchini. Lengo ni kuhakikisha miundombinu hii inakuwa kichocheo cha shughuli za kiuchumi na kuongeza tija katika sekta mbalimbali, hususan kilimo," amesema Profesa Kahyarara.

Ameeleza kuwa sekta ya usafiri wa anga ina nafasi muhimu katika kuwezesha usafirishaji wa mazao ya kilimo kwa haraka na kwa ufanisi, hususan mazao yanayohitaji kufikishwa katika masoko ya mbali kwa muda mfupi, hivyo kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kupata masoko zaidi ndani na nje ya nchi.

TAA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya uendelezaji wa viwanja vya ndege nchini ikiwa ni sehemu ya juhudi za

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.