Na Francisco Peter
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeeleza kuwa uelewa wa watanzania kufungiwa mfumo wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari umeendelea vizuri.
Mwendelezo huo umesemwa unatokana na watu kuendelea kupata, elimu juu ya kutumia mfumo wakufungiwa gesi asilia kwenye magari ni kichocheo cha uchumi wa nchi kukua.
Hayo yamesemwa mwisho wa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Meneja karakana wa taasisi hiyo DIT Prof.Geruti Bosinge.
Bosinge ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa DIT amesema hayo wakati akipambanua elimu juu ya watanzania kuendelea kutumia mifumo ya ufungwaji gesi asilia unaoendelea kutolewa kwenye taasisi hiyo nchini .
"Mihundombinu ya watu kutumia gesi asily inaongezeka siki hadi siku siku taasisi imekuwa kinara katika ufungaji wa mfumo wa gesi asilia kupitia workshop ya taasisi hii,"amesema
Amesema awali walikuwa wakifunga mfumo huo kwenye magari mawili au matatu kwa siku ila kwa sasa kwa siku moja uwezekano ni mkubwa wa kufunga magari matano hadi nane.
Aidha amesema kupanda kwa gharama za mafuta duniani kumechochea idadi ya wanaokuja kuunganishiwa mfumo huo wa watumiaji wa gesi asilia kuongezeka .
Ameeleza kuwa vipo vituo zaidi ya 18 ndani ya jiji la Dar es Salaam vinavyo funga mfumo wa magari yanayotumia gesi asilia ambapo zaidi ya magari elfu 17 ndani ya jiji hili la kwanza kwa ukubwa .
Vilevile ameeleza kuwa hali bajaji kufungiwa mihundombinu hiyo ya gesi asilia inaendelea kupungua huku chanzo kikiwa ni ukuaji wa teknolojia kwa sasa zinakuja zikiwa mfumo huo tayari umewekewa na hivyo kufanya unafuu mkubwa katika matumizi ya mtumiaji.
Hivyo hali hiyo inabadiri matumizi kwenye mfumo wa petrol na kufanya watumiaji wengi kuanza kutumia gesi asilia.
Katika hatua zaidi ya watanzania kufikia mafanikio mengine wadau wameelezwa na taasisi hiyo ya teknolojia ya DIT kuwa gesi asilia ni nishati inayopatikana ndani ya nchi yetu tujenge tamaa atunasababu ya kuacha kutumia gesi yetu.
"Kwa sasa bado sijapata taarifa sahihi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu kujua msgari mangapi yanayotumia gesi yetu asilia ila nafikiria yanaelekea elfu 20 ,"amesema
Kwa upande wake fundi mkuu kwenye karakana hiyo iliyopo kwenye taasisi hiyo ya DIT Agapitus Gurti amesema kuwa kwa mtu anaekuja kunza kwa mara ya kwanza kabla ya kumfungia mfumo wetu wa gesi asilia tunaanza yake kama iko sahihi katika pande zote hasa umeme wagari ndipo tunamshauri afungiwe mfumo.





Hakuna maoni: