DAR ES SALAAM
Makumbusho ya Taifa la Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa maeneo muhimu yatakayotembelewa na wageni wenye asili ya Kiafrika kutoka nje ya nchi, kufuatia ziara maalum.
Ziara hiyo imehusisha wageni kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Diaspora wa Kiafrika (ADDI), inayoongozwa na Mheshimiwa Balozi, Dkt. Arikana Chihombori-Quao kutoka Zimbabwe, ambaye pia ni Mwanzilishi na Rais wa taasisi hiyo.
Ziara hiyo maalum katika Makumbusho ya Taifa imefanyika tarehe 26 Agosti 2026, ikiwa na lengo la kuwapa wageni hao fursa ya kujifunza na kufahamu kwa kina historia, utamaduni na urithi wa Tanzania.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuendeleza diplomasia ya kutangaza utamaduni na urithi wa Tanzania, huku Makumbusho ya Taifa likiwa na nafasi muhimu katika kuhifadhi, kutunza na kuwasilisha historia na utamaduni wa taifa kwa wageni wa ndani na nje ya nchi.
Ziara za aina hii zinatarajiwa kuongeza uelewa na kuvutia zaidi wageni wenye asili ya Kiafrika kutoka mataifa mbalimbali kutembelea Makumbusho ya Taifa, ili kujifunza kuhusu chimbuko, historia, tamaduni na urithi wa Afrika kupitia Tanzania.
Aidha, ziara hiyo inaendelea kuimarisha nafasi ya Makumbusho ya Taifa kama kitovu cha historia, utamaduni na urithi wa Tanzania, pamoja na kuwa daraja muhimu la kuunganisha Tanzania na Waafrika wanaoishi nje ya bara kupitia historia na urithi wao wa pamoja.









Hakuna maoni: