HANSPAUL GROUP YAJINYAKULIA TUZO NNE ZA PMAYA2026

DAR ES SALAAM. 

Kampuni ya Hanspaul Group imeibuka na ushindi wa tuzo nne katika usiku wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Mwaka (PMAYA), zilizofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa The Superdome, Oyster Bay jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimetolewa na Waziri wa Viwanda, Mhe. Judith Kapinga, na kupokelewa na Mkurugenzi wa makampuni hayo, Satbir Singh Hanspaul. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi.

Miongoni mwa kampuni za Hanspaul Group zilizotwaa tuzo hizo ni Dharam Singh Hanspaul and Sons Ltd katika sekta ya Construction, Metal and Metal Products; Hanspaul Industries Ltd katika Paper and Paper Products; Hanspaul Automechs Ltd katika Specialised Motor Vehicles and 4x4 Accessories; pamoja na E-Motion Africa Ltd katika EV Vehicles.

Ushindi huo unaendelea kuonesha mchango wa kampuni hizo katika kukuza uzalishaji wa ndani, ubunifu na matumizi ya teknolojia katika sekta ya viwanda nchini.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.