Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ulaya wa Jamhuri ya Croatia, Mhe. Gordan Grlić-Radman, jijini New York, Marekani, tarehe 25 Septemba 2026, pembezoni mwa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika mazungumzo hayo, Mawaziri hao wamejadili namna ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Croatia, hususan katika biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, kilimo na biashara ya kilimo, uchakataji wa mazao ya chakula, utalii, mafunzo ya kidiplomasia na uwakilishi wa heshima wa kibalozi.
Mhe. Kombo amehimiza wafanyabiashara wa Croatia kuongeza ushiriki wao katika fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania. Pia amependekeza kuimarishwa kwa uwakilishi wa kidiplomasia na kufanyika mara kwa mara kwa mashauriano ya kisiasa kati ya Tanzania na Croatia.





Hakuna maoni: