BUZA YAISHUKURU MERIDIANBET..

DAR ES SALAAM. 

Wakazi wa kata ya Buza, iliyopo wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, wamejikuta kwenye hali ya furaha isiyo na kifani pamoja na kutoa shukrani zake za dhati kwa kampuni ya ubashiri ya Meridianbet baada ya kampuni hiyo kutembelea mtaa wa Kwa Lulenge na kuzigusa baadhi ya kaya kwa kutoa msaada wa vyakula pamoja na bidhaa za usafi. 

Kitendo hiki kimeleta faraja kubwa kwa wakazi wa mtaa huu na kuonyesha kuwa bado kuna taasisi zinazojali jamii kwa vitendo.

Msaada uliopokelewa na wakazi wa mtaa huu umejumuisha mahitaji ya chakula ikiwemo mchele, unga, ngano, mafuta ya kupikia, sukari, na maharage, bila kusahau sabuni za kufulia kwa ajili ya kurahisisha shughuli za usafi. Msaada huu unatarajiwa kusaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto kwa kaya zilizopokea.

Wakazi hawa baada ya kupokea msaada huo hawakuacha kutoa shukrani zao za dhati kwa kampuni hiyo ya Meridianbet, na moja ya mwananchi alikua na haya ya kusema;

“Kwa niaba ya wakazi wote wa mtaa wa Kwa Lulenge, tunamshukuru mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram pamoja na wenzake kwa kututembelea na kutupatia msaada huu wa muhimu kwetu. Uwepo wao umeacha furaha kubwa mioyoni mwetu kwa namna moja ama nyingine na umetupa faraja ya kuona ama kweli tunathaminika.”

“Tunaendelea kuwaomba na watu wengine wenye nafasi ya kurudisha kwa jamii kutukumbuka kwani hali ya maisha kwetu si nyepesi kabisa na uhitaji ni mkubwa sana. Sisi kama wakazi wa Kwa Lulenge tunaahidi kuwa bega kwa bega na wale wote watakaotutembelea, karibuni sana”.

Hili lilikua tukio kubwa na la kipekee ndani ya mtaa huku kwani furaha na tabasamu liliweza kushuhudiwa machoni pa wakazi wa mtaa huu na Meridianbet imefanikiwa pakubwa kuacha alama ya kipekee kwa kila mtu.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.