Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wajane na wanawake waliopoteza waume zao kuwa imara, kusimamia familia zao na kuendeleza miradi waliyoachiwa, akisisitiza kuwa kufiwa hakupaswi kuwa kikwazo cha maendeleo.
Chalamila amesema baadhi ya wanawake hushindwa kuendeleza mali na miradi ya familia baada ya kufiwa na waume zao, huku wengine wakionesha ujasiri kwa kuendelea kusimamia familia na shughuli za kiuchumi.
Ametoa mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa safari yake ya uongozi na kuendelezwa kwa miradi ya maendeleo ni mfano unaoweza kuwatia moyo wanawake kutokata tamaa wanapokabiliwa na changamoto za maisha.


Hakuna maoni: