KILIBA ASISITIZA SIASA ZA HOJA, UKWELI NA UWAJIBIKAJI



  
DAR ES SALAAM. 

Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHILISO), Geoffrey Kiliba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Atetewe, amewataka wanasiasa nchini kutumia majukwaa yao kujenga umoja, mshikamano na maendeleo ya taifa badala ya kuchochea chuki na migawanyiko miongoni mwa Watanzania.

Kiliba amesema tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa sababu ya kujenga uhasama, bali zinapaswa kuwa fursa ya kujadiliana kwa hoja na kuwasilisha mawazo yanayolenga kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya nchi.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kuzingatia ukweli na uwajibikaji katika kauli na matendo yao, akieleza kuwa viongozi wana wajibu wa kulinda umoja wa kitaifa na kuepuka kauli zinazoweza kuongeza tofauti na kutokuelewana katika jamii.

Amesema ujenzi wa taifa unahitaji ushirikiano wa wananchi na viongozi kutoka pande mbalimbali za kisiasa, huku akihimiza kuwepo kwa mijadala yenye staha inayozingatia maslahi mapana ya Watanzania.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.