Moja wa Muda Mrefu Kuhakikisha Usalama na Utii wa Sheria kwa Madereva

Dar es Salaam, 7 Oktoba 2026.

Bolt Tanzania inaendelea kutumia mfumo wake wa muda mrefu wa uhakiki wa utambulisho kupitia picha za moja kwa moja (live selfie) kupitia programu ya madereva, ikiwa ni sehemu ya udhibiti wake wa siku nyingi unaolenga kuhakikisha abiria anachukuliwa na dereva yuleyule aliyesajiliwa na kuhakikiwa kwenye aplikesheni ya Bolt.

Utaratibu huu wa utambulisho ni hatua endelevu na ya msingi ya kiusalama mbali na uhakiki wa nyaraka unaofanyika wakati dereva anapojiunga na Bolt. Akiwa anatumia programu, dereva hutakiwa mara kwa mara kuchukua picha ya moja kwa moja, ambayo hulinganishwa na taarifa za utambulisho wa mmiliki wa akaunti iliyosajiliwa.

Hatua hii inaimarisha udhibiti mkubwa na wa mara kwa mara wa Bolt dhidi ya tabia ya kushirikiana au kubadilishana akaunti, ikihakikisha kuwa mtu anayefika kumchukua abiria ni yuleyule ambaye picha na taarifa zake zinaonekana kwenye programu ya abiria.

Akizungumzia suala hili, Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, alisema kuwa kuendelea kuimarisha na kudumisha uhakiki huu wa utambulisho ni muhimu katika kuongeza uwajibikaji kwenye huduma za usafiri wa mtandao.

“Abiria anapaswa kuwa na uhakika kwamba mtu anayefika kumchukua ndiye yule anayemuona kwenye programu yake ya Bolt. Huyu pia ni dereva aliyesajiliwa, ambaye historia yake ilihakikiwa kabla ya kuruhusiwa kujiunga na Bolt na taarifa zake zipo kwenye kanzidata za mamlaka za usafiri. Uhakiki wetu wa picha ya moja kwa moja umekuwa ukifanya kazi kwa miaka mingi kama kituo kikuu cha utambulisho kinachotusaidia kubaini na kuzuia hali ambapo akaunti ya dereva inatumusiwa na mtu mwingine ambaye si mmiliki aliyesajiliwa.”

Iwapo dereva atashindwa kukamilisha uhakiki huo kwa mafanikio, Bolt huzuia kwa muda matumizi ya akaunti yake wakati ukaguzi zaidi ukiendelea.

Bolt pia inawataka abiria kuhakiki picha na jina la dereva, aina ya gari pamoja na namba ya usajili zinazoonekana kwenye programu na kuzilinganisha na dereva na chombo kilichofika kabla ya kuanza safari. Endapo kuna tofauti yoyote, abiria wanashauriwa kutoa taarifa mara moja kupitia programu ya Bolt.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.