Na Mwandishi wetu,
Morogoro.
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imeendelea kuimarisha uwezo wa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPOs) kupitia mafunzo yanayolenga kuongeza uelewa wa utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44.
Mafunzo hayo ya awamu ya nane yanafanyika Morena Hotel, Morogoro, Oktoba 7 na 8, 2026, yakishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka taasisi za umma na binafsi.
PDPC imeeleza kuwa DPO wana jukumu la kuhakikisha ukusanyaji na matumizi ya taarifa binafsi vinafuata sheria, kusimamia sera za faragha na kushughulikia ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa ndani ya taasisi.
Taarifa binafsi zinazolindwa ni pamoja na majina, namba za simu, barua pepe na namba za utambulisho, huku taarifa nyeti kama afya, benki na alama za vidole zikihitaji ulinzi zaidi.
Kwa mujibu wa Tume, hadi Agosti 2026 taasisi 15,146 zilikuwa zimesajiliwa, huku malalamiko 445 yakipokelewa kuhusu masuala ya ulinzi wa taarifa binafsi.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za PDPC kujenga wataalamu na kuongeza uelewa ili faragha na usalama wa taarifa viwe sehemu ya utendaji wa kila siku wa taasisi.
#PDPC #TaarifaBinafsi #UlinziWaTaarifa #Faragha #UsalamaWaTaarifa



Hakuna maoni: