Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amemhakikishia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Balozi Anda Cristina Filip, kuwa Arusha iko tayari na maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya Mkutano wa 153 wa IPU utakaofanyika nchini Tanzania kuanzia Oktoba 5, 2026.
Akizungumza Oktoba 1, 2026, ofisini kwake jijini Arusha wakati alipokutana na Balozi Anda, Makalla amesema mkoa huo umejiandaa kwa muda mrefu, huku usalama ukipewa kipaumbele. Amesema taasisi mbalimbali zimeendelea kushirikiana kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio.
Amesema mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka mabunge 183 wanachama wa IPU, wakiwemo Maspika 65 kutoka mabunge mbalimbali duniani.
Aidha, Balozi Anda amesema mkutano huo utajadili ajenda mbalimbali za kimataifa, pamoja na uongozi wa IPU na uchaguzi wa Rais mpya wa taasisi hiyo baada ya kumalizika kwa kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa Dkt. Tulia Ackson.
Ameeleza matumaini yake kuwa mkutano huo utafanikiwa na kuwapa washiriki fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini Tanzania.





Hakuna maoni: