Na WMA - Mkuranga_ Oktoba 14, 2026
Wakala wa Vipimo (WMA) imefungua Ofisi wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Japokuwa ofisi hiyo iko wilayani lakini kwa utaratibu wa Wakala wa Vipimo, inatambulika kama Ofisi ya Mkoa wa Vipimo Mkuranga na hivyo inatekeleza majukumu yote kwa ngazi ya Mkoa.
Uwepo wa Ofisi hiyo umeimarisha upatikanaji wa huduma za ukaguzi na uhakiki wa vipimo kwa wananchi na wafanyabiashara wa wilaya za Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia,
Amesema, kwa mfano, wananchi kutoka Kibiti walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 100 kufika Kibaha, hali iliyoongeza changamoto za upatikanaji wa huduma kutokana na umbali na mazingira ya kijiografia.
Msambira ameeleza kuwa ofisi hiyo inatoa huduma mbalimbali, ikiwemo uhakiki wa mizani, vipimo vya ujazo wa gesi, mitungi ya gesi, mizani ya kupimia gesi, uwezo wa kubeba mchanga pamoja na bidhaa zilizofungashwa.
Ameongeza kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi na ongezeko la viwanda katika eneo hilo ni miongoni mwa sababu zinazofanya uwepo wa ofisi hiyo kuwa muhimu katika kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika biashara vinakuwa sahihi na kulinda haki za watumiaji.
Aidha, amesema ofisi hiyo inapokea malalamiko kutoka kwa wananchi, wafanyabiashara na wadau wengine kuhusu udanganyifu wa vipimo, huku akiwahimiza wananchi kutoa taarifa ili hatua stahiki zichukuliwe.
Msambira amesisitiza kuwa wananchi wana wajibu wa kushiriki katika kupambana na udanganyifu wa vipimo kwa kutoa taarifa kuhusu vitendo vinavyoweza kuwaathiri watumiaji na wafanyabiashara wanaofuata taratibu.
Amebainisha kuwa changamoto iliyopo ni baadhi ya wananchi kutofahamu uwepo wa ofisi hiyo au kudhani kuwa haina uwezo wa kutoa huduma zote zinazopatikana katika ofisi za mikoa.
Hata hivyo, amewahakikishia kuwa ofisi ya Wakala wa Vipimo Mkuranga ina uwezo wa kutoa huduma za uhakiki na ukaguzi wa vipimo ndani ya eneo lake la mamlaka, bila wananchi kulazimika kwenda maeneo mengine.
Ofisi hiyo ipo Mkuranga B, katika Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, na wananchi wamehimizwa kuitumia kupata huduma na kutoa taarifa zinazohusu ukiukwaji wa taratibu za vipimo.



Hakuna maoni: