DAR ES SALAAM
Sekta ya majengo na makazi jijini Dar es Salaam inatarajiwa kupata msukumo mpya kupitia mradi wa Keyne Centre unaotekelezwa eneo la Victoria, ukiwa na jumla ya ghorofa 26 na nyumba zenye ukubwa wa kipekee.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Crate Estates, Aidan Anacreth, amesema jengo hilo linalomilikiwa na Asiano Global Investment Company Limited, linatarajiwa kuwa refu zaidi kando ya Barabara ya New Bagamoyo, huku likijipambanua kwa kuwa na nyumba kubwa zaidi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa maelezo ya mradi yaliyotolewa na Mr. Jack, Mkurugenzi wa Ubunifu wa Uhandisi (Director of Engineering Design), jengo hilo litakuwa na ghorofa tisa za mwanzo zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za kibiashara, huku ghorofa zinazofuata zikitumika kwa ajili ya makazi.
Keyne Centre itakuwa na nyumba zenye vyumba vitatu, vinne na vitano, huku nyumba yenye ukubwa mdogo zaidi ikiwa na eneo la mita za mraba 221. Kila nyumba itakuwa na balcony mbili au zaidi zitakazowawezesha wakazi kufurahia mandhari ya bahari na maeneo mbalimbali ya jiji.
Huduma nyingine zitakazopatikana katika jengo hilo ni ukumbi wa mazoezi, bwawa la kuogelea, maeneo maalumu ya maegesho ya magari pamoja na teknolojia ya kisasa ya maonesho ya picha za pande tatu (3D Visual Displays).
Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Julai mwaka huu, ambapo sehemu ya biashara inatarajiwa kukamilika mwezi Mei, huku jengo lote likitarajiwa kukamilika Februari 2028. Crate Estates inasimamia mauzo na utangazaji wa mradi huo, huku Witness Natai akiwa Meneja Mauzo.
Wananchi na wadau mbalimbali wanakaribishwa kutembelea eneo la mradi huo lililopo Victoria ili kujionea maendeleo ya ujenzi na kupata maelezo zaidi kuhusu fursa za uwekezaji na makazi bila malipo ya kiingilio.
#KeyneCentre #CrateEstates #RealEstateTanzania #DarEsSalaam #UwekezajiWaMajengo





Hakuna maoni: