VYAMA VYA SIASA VIMETAKUWA KUJIBUSHANA KWA HOJA ZENYE MASHIKO.




Dar es salaam,

VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kusikulizana,kupinga na kujadiliana kwa hoja kwajili ya kujenga vyama vyao,ikiwa ni pamoja na kupeana fursa ya kutoa maoni yakuboresha na kuimarisha Demokrasia nchini.

Wito huo umetolewa leo Julai 17, 2023 na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed, wakati akifunga Kikao kazi cha viongozi wa vyama vya siasa nchini uliolenga kutoa maoni juu ya uchaguzi na maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki wa vyama vya siasa.

Aidha amesema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inathamini mchango wa Vyama na wanasiasa na kuahidi kufanyiakazi maoni yote yaliyotolewa katika Kikao kazi hicho.

"Haijalishi umetoa maoni kwa sauti gani,iwe ya ukali,pole,ya kugombeza, sisi tutajali kile unachokisema na tutazingatia na kukifanyia kazi kwa umakini mkubwa"amesema Mohamed.


Kwa upande wake Makamu mwenyekiti (Bara) Dorothy Semu amesema kikakao kazi kimetoa fursa nzuri kwa Viongozi wa Vyama na Watendaji Wakuu kupata Elimu na kubadilisha mawazo kupitia maoni mbalimbali na kuweza kuboresha na kuksbiliana changamoto mbalimbali za kisiasa ndani na nje ya Chama pia kikao hicho kimetoa fursa kwa Vyama kuona ni kwa jinsi gani wamefuata sheria na kanuni zilizopo.



Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba amesema bado ana wasiwasi mkubwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongozi mwaka 2024 kutokana ns taratibu za kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki bado haujaandaliwa, hivyo kuiomba serikali kuandaa utaratibu mzuri usiongiliwa na mamlaka nyingine na kuuitia Doa uchaguzi huo.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.