Dar es salaam,
Na Emmanuel Kawau.
Akizungumzia na Waandishi wa Habari katika Banda la Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kwenye Maonyesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja Jiji Dar es salaam Makamu Mkuu wa Chuo Prof Lughano Kusiluka amewakaribisha watu wote kutembelea katika banda lao na kupata taarifa mbalimbali kuhusu UDOM pia kuweza kupata fomu za kujiunga na chuo hicho.
"Tumekuja hapa kwaajili ya kuwaelimisha wale wanaotaka kujiunga na Chuo namna ya kuingia kwenye mfumo wa kujisajili na kujiunga na kuweza kuchagua program ambazo mtu unazihitaji na tunawataalamu wetu kwenye Banda hili kubwa kuliko mabanda yote katika maonyesho haya na hiyo inatafsiri ukubwa wa UDOM"
"Niwakaribishe wote Chuo Kikuu Cha Dodoma kwaajili ya kusoma kwasababu hakuna fani ambayo inafundishwa katika nchi hii kwasasa ambayo huwezi kuipata katika Chuo Kikuu Cha Dodoma"
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Lughano Kusiluka akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi waliopo katika maonyeshesho hayo.
Prof Lughano ameendelea kwa kusema "Tunawatayarisha vijana wetu kwaajili ya kujiajili baada ya kumaliza masomo yao,wote tunajua kwamba fursa za ajira sio nyingi lakini fursa zipo kama na wewe unaesoma unajihesabu kama mmoja wapo wanaoweza kutengeneza fursa za ajira kwaajili yako mwenyewe lakini na kwaajili ya watu wengine".
Prof Kusiluka ameongeza kuwa kupitia maonyesho hayo pia wanatoa taarifa mbalimbali ikiwemo kuhusu utafiti,machapisho,na maendeleo ya teknolojia "sasa hivi mnasikia kuhusu Artificial intelligence (Akili mnembo) imefika mahali inaanza kutuchanganya ila pale UDOM tunaowataalamu na siku za hivi karibu tutaanza kutoa kozi fupi ili watanzania waweze kuijua Akili bandia ambayo inatikisa Dunia kimaendeleo badala ya kuteseka nayo tujitayarishe kuitumia kwasababu imetukuta na sisi hatuwezi kuikimbia".
Aidha amebainisha kuwa UDOM imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali hususani katika Tehama na Sheria ambapo wamekuwa washindi katika Mashindano mbalimbali Barani Afrika.


Hakuna maoni: