Dodoma.
Umoja wa Afrika (AU) waridhia kwa kauli moja kupitisha jina la Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson kuwa mgombea wao katika Umoja wa mabunge ya Duniani (Inter-Parliamentar Union -IPU).
Taarifa iliyotolewa Ofisi ya Bunge kitengo cha mawasiliano imeeleza kuwa, uamuzi wa kupitisha jina la Dk Tulia ulitokana na ombi la Tanzania la kuungwa mkono kwenye mkutano huo Uliofanyika July 13,2023 Jijini Nairobi nchini Kenya.
"Dkt Tulia Ackson ameungwa mkono na Bunge la Afrika (PAP), Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Jukwaa la mabunge ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC-FP) ili kugombea nafasi hiyo" Imeeleza Taarifa hiyo ya Bunge.
Uchaguzi wa Rais wa Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) unatarajia kufanyika Oktoba 27, 2023 nchini Angola ambapo Afrika itamsimamisha Dk Tulia Akson kugombea nafasi hiyo.

Hakuna maoni: