Dar es salaam,
Na Emmanuel Kawau.
Biteko ameyasema hayo Julai 19,2023 Jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wachimbaji wakubwa wa Madini Nchini kupitia( Tanzania Chamber Of Mines) ,Waziri Biteko amesema kuwa serika itahakikisha inaondoa changamoto ambazo zinawafanya wachimbaji madini washindwe kufanya shughuli zao kwa urahisi pia amesema maeneo ambayo yatafanyiwa kazi ni pamoja na Miundombinu ya Umeme na Barabara zinazoingia Migodi.
" Leo tumeamua kufanya Mkutano nao ili kujadili changamoto na kuwambia kitu gani serikali imekusudia kukifanya kutoka kwao,ambapo moja ya Changamoto ni Changamoto za Kodi,usimamizi na tulipomaliza bunge la bajeti baada ya serikali kupitisha Muswada wa fedha(financal bill) mambo mengi yameweza kutatuliwa" amesema Biteko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Mines,Mhandisi Filbert Rweimamu amesema kuwa chemba ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi ni lazima kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya Mkusanyiko wa hiari wa watafiti,wachimbaji na watoa huduma katika sekta ya Madini.
"Mkutano wa leo ambao tumekua tukifanya kila robo mwaka tumejaribu kutoa taarifa muhimu za maendeleo ya shughuli zetu pamoja na kueleza umma na kuiambia serikali vitu gani ambavyo vinaweza kurahisisha shughuli zetu za uzalishaji wa madini tunategemea sana kama ilivyoaksiwa ifikapo mwaka 2025 sekta ya Madini iweze kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la Taifa". amesema Mhandisi Rweyemamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tembo Nickel Benedick Masunzu amesema katika Mradi wao wa uchimbaji wa Madini aina ya Nickel fedha ni muhimu zaidi nakwamba tayari kampuni hiyo imefanikiwa kupata kiasi cha fedha kitakachosaidia kuanza uzalishaji wa madini hayo ifikapo mwaka 2026.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Faru Ghraphite ambayo inatarajia kuanza kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) katika Mkodi wa Mahenge amesema baadhi ya Changamoto ni Kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika kwenye Migodi lakini changamoto ambayo inapatiwa suluhisho kwasababu wapo katika mazungumzo na TANESCO.
Pia amesema Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania( BOT) wameweza kutafuta masuluhisho mbalimbali katika kutatua changamoto za kifedha kwani wao ndio Wadau wakubwa katika Mradi huo.
" Kwa kiasi fulani tumepata mafanikio mazuri,mpaka leo tulipo angalau bado kuna mambo mawili,matatu ambayo yanatakiwa kutolewa ufafanuzi katika sheria hii ya fedha ya mwaka 2023 iloyotolewa hivi karibuni.
Baadhi ya Wadau na Wachimbaji wakubwa wa Madini wakisikiliza kwa makini mada na mawasilisho mbalimbali.







Hakuna maoni: