JEZI ZA SIMBA SC KUZINDULIWA KILELENI MWA MLIMA KILIMANJARO.


SIMBA DAY KUFANYlKA AGOSTI 6,MWAKA HUU.



Dar es salaam.

Simba SC hii leo imesema itazindua jezi zake kileleni mwa mlima Kilimanjaro siku ya ijumaa Agost 21,2023 pia imetangaza rasmi kuwa tamasha lake la Simba Day linatarajiwa kufanyika Agosti 6,2023.

"Nawambia rasmi hapa kwamba jezi ya Simba itazinduliwa juu ya Mlima Kilimanjaro,Jezi itaanza kupandishwa mlimani siku ya Jumatano na watakuwa kileleni siku ya Ijumaa saa 1:00 usiku jezi itakuwa imefika kileleni na Jumamosi jezi itakuwa kwenye maduka yote nchini."- Imani Kajula,Mtendaji Mkuu wa Klabu.

Aidha Kajula amesisitiza kuwa wataendelea kuzindua jezi zeo katika njia tofauti,"sisi tunafanya vitu tofauti haijawahi kutokea".

Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally Amesema wameamua kufanya Tamasha la Simba Day Agosti 6,ili kutoa nafasi kwa wachezaji wa timu hiyo kupumzika na kujiaanda kwaajili ya mchezo wa Ngao ya hisani Agosti 10 mwaka huu.


"Tulitaka Tamasha la Simba Day tulifanye Tarehe 8,mwezi wa 8,2023 kwasababu ndiyo tarehe rasmi ya Mmnyama lakini tarehe 10 tunakwenda Tanga kwenye mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Singida kwahiyo tukicheza tarehe 8 Simba Day maana yake tarehe 9, tunatakiwa kusafiri ili tarehe 10 tucheze mechi".


Ahmed ameendelea kueleza kuwa "Japo tumfunga Singida Insha-Allah, lakini Lazima Wachezaji wapate muda wa kupumzika"


"Kwa kuzingatia hilo tukaamua kurejesha nyuma siku ya Mchezo wetu kwahiyi simba Day itakuwa siku ya Jumapili ya tarehe 6 mwezi wa nane mwaka huu nakatika Tamasha letu Tiketi zitakuwa katika bei rafiki"Amesema Ahmed.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.