ACB BANK KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA BANK NCHINI.



Dar es salaam,

Na Mwandishi wetu.

Akiba Commercial Bank Plc( ACB) imesema itahakikisha inaendelea kujikita katika kuleta mapinduzi ya utoaji huduma bora za kibenki nchini Tanzania kwa kuboresha huduma zake ikiwemo kuweka fedha na kutoa fedha pia kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa Watu wote .

Akizungumaza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam na Waandishi katika maonyeshoa ya 47 ya Biashara Sabasaba katika banda la Bank hiyo Mkurugenzi Mtendaji Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi amesema kuwa ACB imeboresha huduma zake ambazo zitakuwa chachu ya kukidhi matarajio ya wateja waliopo pamoja na wateja watarajiwa katika kujipatia huduma.

Hata hivyo amebainisha kuwa Maboresho makubwa yamefanywa kwa huduma za wateja binafsi,(Personal banking) ambayo inawalenga Waajiriwa wa sekta za Umma na sekta binafsi ambapo mteja anaweza kupata mikopo ya aina mbalimbali kuendana na mahitaji yake mathalani huduma za mikopo ya kujenga na kuboresha makazi, pia mikopo ya muda mfupi (Salary advance) kwa ajili ya kutatua dharura za kifedha kwa muda mfupi. 

"Benki imezidi kuboresha huduma za mikopo kwa wateja wakubwa , (Corporate customers),wakati,na wadogo kuendana na mahitaji ya soko na tunatoa huduma za bima kwa wajasiriamali pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya bima –IPF (Insurance Premium Financing)" Amesema Mkurugenzi

Sambamba na hayo Arumasi amebainisha kuwa ACB imeboresha huduma zake kwa kupitia Mawakala wake (Akiba Wakala) na simu ya mkononi (Akiba Mobile) pia imeboresha mifumo ya utumaji pesa kwenda nje ya nchi.

Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo na amewashukuru kuchagua ACB Bank kwa kutumia huduma zake ikiwemo wafanyakazi ,Wajasriamali hivyo amewasisitiza waendelee kupata huduma bora kwani ni Benki sahihi na bora inayolenga kutimiza malengo ya Wateja wake.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.