TULIVU SPACE KUJA NA TAMASHA LA KIPEKEE APRIL 20/2024.



DAR ES SALAAM.

Taasisi ya Utulivu Space inatarajia kufanya uzinduzi wa Tamasha linalijulikana kama Utulivu Experience lenye lengo la kuwaletea pamoja watanzania kwa ajili ya kufurahia Utulivu na amani ambayo ni tunu ya Taifa tangu Tanzania ipate Uhuru.

Hayo yameelezwa Leo Jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Ibrahim Rwegerera wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelezea uzinduzi wa Tamasha hilo ambalo litafanyika April 20 mwaka katika ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini humo.

Aidha amesema kuwa Tamasha hilo litawahusisha watu wa kada mbalimbali ikiwemo watu maarufu, viongozi na wenye matokeo chanya Ndani ya Jamii.

Ameongeza kuwa waalikwa katika tamasha hilo watapata fursa ya kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali ikiwemo wastaafu na wale waliosaidia katika kudumisha amani na mshikamano wa Taifa.

Amesema anaamini kuwa kupitia Tamasha hilo Tanzania itasherehekea faida za amani na Utulivu ambayo Moja ya alama inayolitambulisha taifa la Tanzania Duniani kote.

“Utulivu Experience ni jukwaa ambalo limetengenezwa kwa Neema za Mungu kufurahia amani na Utulivu wa Tanzania toka enzi za Wazee wetu ambao tunategemea kupata uzoefu wa njia walizotumia kudumisha amani ambayo mpaka leo tunayo” Amesema Rwegerera.

Sambamba na hayo amebainisha kuwa Tamasha hilo litakuwa na kiingilio kwa makundi matatu ambapo sehemu ya watu wa kawaida ni shilingi 270,000, VIP ni 1,350,000 na VVIP 2, 270,000.

Kwa upande wake Mshauri wa Tamasha hilo Antony Luvanda amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kuwaomba watanzania na raia wa nchi jirani kujumuika pamoja kuendelea kudumisha amani na Utulivu.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.