Dar es salaam.
Umoja wa Vyama 13 vya siasa vimesema havikubaliani na njia ambayo chadema imeamua kuichukua kwa kufanya maandano hapo January 2024 kwani hatua hiyo wameichukulia na kuiita kama ni ubinafsi mkubwa na kuona kila walitakalo wao ni sahihi na linapaswa kufuatwa.
"Tufanye siasa za hoja tusigusane maungoni tujenge hoja tujibu kwa hoja"
Kupitia vikao mbalimbali vya baraza la vyama vya siasa wamekuwa wakijadiliana na kuhakikisha wanajiepusha na maandano na kujikita zaidi katika kutoa hoja zenye mashiko.
"Wao tokea awali waligomea kuhudhulia katika vikao vya baraza bado wapo nyuma maswala ya maandano tumeshaacha zamani sana lakini kwakuwa wao walikuwa haudhulii hawajui nini kilifanyika"
"Kama katika mfumo huu wa democrasia tutaendelea kupingana hatitaweza kufika tutakako, ni lazima tuweke maslai ya wananchi mbele ili kuwa na Taifa lenye maendeleo thabiti" Amesema Mluya
Katika mswada wamekubaliana kuondoa halinya kupita bila kupingwa, kuondoleqa kwa hali ya kusema umekosea baadhi ya vipengele katika kujaza fomu za uchaguzi,
Karibia 60% ya maoni yamechukuliwa lakini si kila maoni yamechukuliwa vyama 13 vimekili wazi.
Wameiomba Serikali kuona umuhimi wa vyama vya siasa visivyopata ruzuku kuanza kupatiwa na wao ili kuweka usawa kwenye uwanja wa kiasasa.
Wanawasii viongozi wenzao kuendelea kutumia njia sahihi zilizopo ikiwemo mahakama,baraza la vyama,msajili wa vyama ilinkufikia mabadiliko ikiwemo kushirikiana na wengine na kuacha tabia ya kupinga kila kitu.
Wameiomba Serikali kuzingatia maoni ya vyama vya siasa, viongozi wa dini na watu mbalimbali ambao wamejitomeza kutoa maoni juu yaaboresho ya sheria ya uchaguzi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha ADC Doyo Hassan Doyo amesema wanaiomba serikal kutotishika na maandano ya chama kimoja kwaajili ya faida ya wengi.Vyama hivyo 13 vilivyotoa tamko hilo ni pamoja na DP,NRA,UDPD,ADC, DEMOCRATS MAKINI,NLD,TLP,SAU,UD,CCK,AFD,ADA TADEA,
Hakuna maoni: