ZAIDI YA 1,069 ZIMERIDHIA NA KUJIANDIKISHA KUHAMA KATIKA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO.



Na Mariam Muhando,

Arusha.

Hadi kufikia Januari 12, 2024 Zaidi ya kaya 1069 zimejiandikisha kuhama kwa hiari katika eneo la hifadhi ya ngorongoro, Ikiwa takribani kaya 633 zenye Watu 3526 na mifugo zaidi ya elfu 16 hadi kufikia tarehe hiyo tayari zimeshahama kwenye maeneo mbalimnali yaliotengwa na Serikali ikiwemo Msomera iliopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga.


Zoezi la kuwahamisha Wakazi hao limetokana na agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassani Katika kuhakikisha Wananchi waliokuwa wakiishi Ngorongoro wanapata huduma balimbali za kijamii l ambapo awali walikuwa hawazipati huduma hizo kutokana na changamoto ya kuishi ndani ya Hifadhi hiyo.


Akizingumza na Waandishi wa Habari Kamishna msaidizi wa uhifadhi ,Mipango ufuatiliaji na Tathmini kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Lilian Magoma mara Baada Serikali kuamua Waandishi hao watembelee Hifadhi hiyo Kwa lengo la kujionea hali halisi ya maisha ya Wananchi hao na kuelekea kwenye maeneo yaliotengwa na Serikali ikiwemo ambapo Wakazi wa eneo hilo wanaishi Katika Mazingira hatarishi ya kuishi na Wanyama wakali sambamba na kutopiga hatua kiuchumi.


Magoma amesema wanaendelea na zoezi la kuwahamisha Wananchi hao Kwa kufuata taratibu mbalimbali za Kisheria bila ukiukwaji wa haki za binadamu." Kwani tumezingatia sheria na utu katika kuwahamisha hata hivyo nawasisitiza wananchi wa Ngorongoro kuhama sehemu hii kwani kuna faida kubwa ikiwemo kulinda Hifadhi.


Nae Afisa Uhifadhi Mwandamizi kutoka NCAA,Kassim Nyaki,amesema mwaka huu wameanza kutekeleza zoezi hilo wameanza kujenga nyumba 5000 katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro ikiwemo eneo la Msomera,Kilindi pamoja kitwai mkoani Manyara.


Nyaki amsema kwa sasa kila wiki wanahamisha watu na kuwapeleka Msomera Handeni Mkoani Tanga ambapo Kwa Sasa muamko umeongezeka wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kuhama baada ya kuelimishwa ambapo hamasa ni kubwa sana.h


"Changamoto iliyopo ni mwananchi akijiandikisha leo anataka kuhama leo na hii imetokana na Serikali kuwapa uhuru Wananchi wa Ngorongoro kuchagua sehemu wanayotaka kwenda na sio kuchaguliwa sehemu".

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.